Ressources numériques en sciences humaines et sociales OpenEdition Nos plateformes OpenEdition Books OpenEdition Journals Hypothèses Calenda Bibliothèques OpenEdition Freemium Suivez-nous

Catégorie : Tanzania 2025: Muendelezo wa ukandamizaji wa serikali

Mfululizo huu wa makala ya Mambo! unajikita katika kuelezea mwaka wa uchaguzi wa 2025 nchini Tanzania. Unatoa maelezo ya kipekee wa usomaji wa kina na ukaribu wa vielelezo vya matukio ya kisiasa ya mwaka huu wa uchaguzi, uliokua na matukio mengi na uliotawaliwa na muendelezo wa ukandamizaji wa serikali. Katika kila sehemu cha mfululizo huu, tukio lililochaguliwa linazalishwa tena katika asili yake na kutafsiriwa panapohitajika, likiwekwa katika muktadha kwa uangalifu na kufafanuliwa au kupewa maelezo ya karibu kwa lengo la kutoa ufafanuzi wa kuelewa kwa kina sehemu lilipotokea pamoja na maana na umuhimu wake. Matukio haya ni vyanzo ama nyaraka ya maana kwa ajili ya kuchambua muendelezo wa utawala wa kimabavu na ukandamizaji wa wazi uliofanywa na serikali ya Tanzania katika kipindi hiki cha uchaguzi mwishoni mwa mwaka 2025.

Sehemu ya #5. ‘Kura ni alama ya maendeleo’: Kuahidi maendeleo Zanzibar kupitia kampeni zilizotawaliwa na mabango ya kisiasa

Marie-Aude FOUÉRÉ, Nicodemus MINDE, Mambo!, no. 110, 2026.
Katika uchaguzi wa Zanzibar wa mwaka 2025, maendeleo haikuashiria tu ‘maendeleo’—yalitumika kama teknolojia ya kisiasa (political technology) ambayo kupitia kwayo CCM (Chama cha Mapinduzi) ilijaribu kugeuza miundombinu kuwa uhalali wa kisiasa na kupiga kura kuwa kitendo cha utii uaminifu badala ya chaguo la wazi. Kama ilivyo kwa dhana yoyote, na hasa kwa dhana ambayo, kote Tanzania (ikiwemo Zanzibar), inabeba uzito wa historia ya ukoloni na ya baada ya ukoloni, maendeleo yana maana nyingi na zinazotegemea muktadha.

Sehemu ya #4. Jinsi vyombo vya habari vya Kenya vilivyoripoti mwelekeo wa Tanzania katika ukandamizaji wa serikali kupitia vichwa vya habari vya gazeti la The Standard (29 Oktoba–10 Novemba 2025)

Marie-Aude FOUÉRÉ, Nicodemus MINDE, Mambo!, no. 109, 2026.
Kwa siku nane mfululizo, kuanzia siku ya kupiga kura (Jumatano 29 Oktoba 2025) hadi siku mbili baada ya sherehe rasmi ya kuapishwa kwa rais mpya wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kurasa za mbele za gazeti la kila wiki la Kenya The Standard zilifuatilia kwa karibu kile kilichoelezwa kuwa kushuka kwa hatua kwa hatua kuelekea ukandamizaji wa serikali katika kipindi hiki muhimu cha upigaji kura na siku za mwanzo baada ya uchaguzi mkuu wa Tanzania wa 2025.

Sehemu ya #3 Miili ya kigeni, vijana waliopotoshwa: Hotuba ya kuapishwa kwa Samia Suluhu Hassan, 3 Novemba 2025

Nicodemus MINDE, Marie-Aude FOUÉRÉ Mambo!, no. 108, 2026.
Jumatatu tarehe 3 Novemba 2025, sherehe ya kuapishwa kwa Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Tanzania ilifanyika katika uwanja wa gwaride la kijeshi mjini Dodoma, mji mkuu wa Tanzania, siku mbili tu baada ya ushindi wake kutangazwa. Mtandao wa intaneti, ambao ulikuwa umezimwa tangu siku ya kupiga kura (29 Oktoba), ulianza kurejeshwa katika hali yake ya kawaida taratibu. Tanzania ilikuwa imeanza kurejea katika hali yake ya kawaida baada ya kuwa gizani kwa wiki moja – ilikuwa kama kuzimu.

Sehemu ya #2 Kuchora fedheha ya kimaadili ya Samia Suluhu Hassan: Katuni ya kisiasa ya Gado ya tarehe 1 Novemba 2025

Marie-Aude FOUÉRÉ, Nicodemus MINDE, Mambo!, no. 107, 2026.
Mnamo tarehe 1 Novemba 2025, katuni ya mchoraji Gado iligusa hisia za wengi. Ilimuonyesha rais mteule wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akiapishwa mbele ya Jaji Mkuu, mmoja wa mikono yake ukishikilia Qur’ani, na mwingine ukiwa juu ya Katiba, akiwa amesimama juu ya lundo la maiti zenye damu ambazo zulia lililozifunika halifanikiwi kuzificha. Mikono ya rais mteule, nguo zake, na hata Qur’ani yenyewe zimechafuka kwa damu. Wanaume wenye silaha wenye sura kali, nyuso zilizofunikwa na skafu na kofia za bereti zilizokuwa na alama ya fuvu la kichwa wanamlinda rais na kuhakikisha usalama wa sherehe ya uapishwaji.

Sehemu ya #1. Hotuba ya Tundu Lissu ya tarehe 3 Aprili 2025, “Tutakinukisha: ‘Hakuna Mabadiliko, Hakuna Uchaguzi’”

Nicodemus MINDE, Marie-Aude FOUÉRÉ, Mambo!, no. 106, 2026.
Tarehe 21 Januari 2025, Tundu Lissu alimshinda Freeman Mbowe katika uchaguzi wa ndani wa CHADEMA (Chama Cha Demokrasia na Maendeleo) na akawa mwenyekiti mpya wa chama. Maswali mawili muhimu yaliibuka mara moja: Je, chama kingeweza kustahimili mabadiliko haya kutoka kwa Mbowe, mwanasiasa mzoefu aliyekuwa kiongozi wa chama kwa zaidi ya miaka ishirini na mtetezi wa hali ya kisiasa iliyokuwepo (status quo), hadi kwa Lissu, anayejulikana kama kiongozi mwenye msimamo mkali (Minde, 2024)? Na chama tawala cha muda mrefu CCM (Chama Cha Mapinduzi), ndani ya mfumo wa chama kimoja wa kiimla (Makulilo, 2008; Paget, 2019), kingejibu vipi?